

6 March 2025, 11:25 pm
Kuelekea kilele cha maadhisho ya wanawake duniani 2025, serikali imetoa fedha zaidi ya milioni tatu katika halmashauri ya wilaya ya uvinza kwa ajili ya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu ambapo wanatakiwa watumie katika kuleta maendeleo.
Na Theresia Damasi
Kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani,wanawake wilayani uvinza mkoani wameaswa kutumia fursa ya mikopo inayotolewa na halmashauri ili kujikomoa kiuchumi huku akina baba wakitakiwa kuwaunga mkono wake zao.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa wilaya ya uvinza Dinah Mathamani ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya maadhisho ya wanawake yaliyofanyika katika viwanja vya Kachiringuru kata ya uvinza.
Dinah Mathamani amesema kulingana na kauli mbiu ya siku ya wanawake 2025 inayosema” Wanawake na wasichana 2025 Tuimarishe Haki,Usawa na Uwezeshaji” ambapo amesema wanawake wanamchango mkubwa katika jamii ikiwa ni pamoja na walezi katika familia, washauri na wachapa kazi hivyo wanatakiwa kupewa heshima yao.
Sauti ya Dinah 1…………..
Ameendelea na kusema kuwa mwaka 2025 serikali imetoa fedha zaidi ya milioni tatu katika halmashauri ya wilaya ya uvinza kwa ajili ya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu ambapo wanatakiwa watumie katika kuleta maendeleo na sio vinginevyo.
Sauti ya Dinah 2……………
Sanjari na hayo Mkuu huyo wa wilaya ya uvinza Dinah Mathamani amesema kutokana mabadiliko ya tabia nchi jamii inapaswa kutunza mazingira ikiwa ni pamoja kutunza misitu na kutumia nishati safi ambayo ni gesi.
Nao wanawake waliohudhuria maadhimisho hayo wameishukuru serikali kwa kuwapa elimu juu ya matumizi sahihi ya nishati jambo ambalo linasaidia katika kutunza mazingira.
Pamoja na hayo Mkuu wa wilaya uvinza Dinah Mathaman ameeleza umhimu wa siku ya wanawake duniani na historia yake ambapo wanaume wanajukumu la kuwaunga mkono wanawake na wasichana.
Sauti ya Dinah 3………