

26 February 2025, 11:48 am
Mtendaji wa kata ya uvinza awasihii wananchi kutumia sanduku la maoni kuziwasilisha kero zao pamoja na mapendekezo yao.
Na Linda Dismas
Wananchi wa kata ya Uvinza wameaswa kutumia sanduku la maoni kwa kuwasilisha kero zao.
Hayo yameelezwa na Afisa mtendaji kata ya Uvinza Bw.Edward Amos wakati akifanya mazungumzo na Uvinza fm ofisini kwakwe na kusema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa mwananchi kutumia sanduku la maoni kwaajili ya kuwasilisha maoni yake.
Aidha Bw. Amos amesema kuwa kupitia maoni yanayowekwa kwenye sanduku kunawasaidia wao viongozi kutambua ni changamoto gani wanazokumbana nazo wananchi.
Pia amewataka wananchi wa kata ya Uvinza kuwa na mazoea ya kutumia sanduku la maoni ili kufikisha mapendekezo na changamoto zao kwa viongozi.