Uvinza FM

Imani potofu na uchache wa vituo kudhoofisha zoezi la utoaji chanjo

29 September 2021, 6:40 pm

Na,Glory Paschal

KIGOMA

Imeelezwa kuwa Imani  Potofu na uchache wa vituo vya kutolea chanjo katika maeneo ya jamii imeelezwa kuwa chanzo cha kudhoofisha zoezi la utoaji chanjo ya UVIKO 19 kutofanikiwa mkoani Kigoma

Hayo yamebainishwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt. SIMON CHACHA wakati akizungumza na waandishi wa habari na kueleza elimu ya umuhimu wa chanjo ya UVIKO 19 na kuongeza kuwa hiyo kasi ya utoaji chanjo haikuwa kubwa

Sauti ya Mganga mkuu mkoa wa Kigoma

Aidha Dkt CHACHA amesema sekta ya afya imeamua kuboresha miundombinu yote itakayofanikisha jamii nzima ya Kigoma kufikiwa  na  wahudumu wa afya wanaotoa chanjo ya UVIKO 19 ikiwemo kutoa elimu kwa makundi maalumu

Sauti ya mganga mkuu wa mkoa wa kigoma

Baadhi ya waandishi wa habari akiwemo DEOGRATIUS NSOKOLO  ambaye ni Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) amesema kutokana na shughuli za wanahabari ni muhimu kupata elimu ikiwemo ya chanjo kutokana na wao kuwa sehemu hatarishi ya kupata virusi hivyo.

Sauti ya Rais wa umoja wa klabu za waandishi Tanzania