Uvinza Fm

Serikali kuja na mpango harakishi wa kila mwananchi kupata chanjo

27/09/2021, 6:48 pm

Na, Mwanaid Suleiman

Serikali  imesema imekuja na mpango harakishi wa kuhamasisha  chanjo  ya corona ikiwa lengo ni kuhamasisha kila mwananchi anapatiwa chanjo ya corona

Hayo yamesemwa na  DR CRESENCIA JOHN kutoka ofisi ya mganga mkuu mkoani kigoma wakati akizungumza na kipindi cha amka na redio uvinza fm  ambapo amesema mpango huo uanweza kuwafata wananchi nyumba kwa nyumba

Sauti ya DR.Cresencia

Kwa upande wake DR. HOSEA WILIAM amesema kuwa wamejipanga vyema kuelimisha  wananchi kwa wale ambao hawana uelewa  juu ya chanjo ya corona

Sauti ya Dr. Hosea

kwa mkoa wa kigoma chanjo ilizinduliwa tarehe 3 mwezi 8 huku uitikiaji wa uchomaji  chanjo ukiwa bado ni hafifu , ikiwa hadi  sasa watu waliojitokeza kuchoma chanjo kwa mkoa  wa huu ni watu 5913 na  kwa wilaya uvinza ikiwa ni 651.