Uvinza Fm

Wanafunzi wa kike waiomba serikali kuwaletea walimu wa kike mashuleni ili kutatuliwa changamoto zao

25/08/2021, 5:56 pm

Na,Christina Daud

Baadhi  ya Wanafunzi wa kike katika shule ya sekondari nguruka wilayani uvinza mkoani kigoma wanapata changamoto ya kuwa na walimu wa kike wa kutosha mashuleni kwa ajili ya kueleza shida zao hususani suala la hedhi wanapokua shuleni

Wakizungumza na redio uvinza fm  wamesema   wakiingia katika mzunguko huo kuna wengine  wanashindwa kuendelea na vipindi  vya  darasani kutokana na changamoto mbali mbali ikiwemo kuogopa kuwaambia walimu wa kiume  pindi wanapokuwa katika hali hiyo .

Sauti za wanafunzi

Nae  mwalimu matroni wa shule hiyo GLADSY WALUHIGA amesema wanafunzi wa kike wanatakiwa kuwa huru wasiwe waoga katika kuwaelezea walimu wa kiume matatizo yao kwani nao pia ni waelewa.

Sauti ya matron

Aidha watoto wa kike ambao tayari wameshaingia katika hali ya kupata hedhi hawatakiwi kuwa waoga kuzungumza na wazazi wao pamoja na walimu wa kiume pindi wanapokuwa katika hali hiyo.