Tujifunzeni lugha ya alama tuwasaidie watu wenye uziwi
2 October 2024, 8:36 am
Na Vuai Juma.
“Upo umuhimu mkubwa wa kujifnza lugha ya alama ambayo ndio kiunganishi kikubwa kwa watu wenye ulemavu wa uziwi”.
Na Vuai Juma.
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Harusi Said Suleiman, amesema serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kutoa kipaumbele katika kutoa mafunzo ya lugha ya alama kwa lengo la kuwasiliana na watu wenyechangamoto ya usikivu.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la watu wenye ulemavu Zanzibar, Mhandisi Ussi Khamis Debe wakati akizungumza kwa niaba ya Waziri huyo, katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya viziwi Duniani yaliyofanyika Jongowe Wilaya ndogo Tumbatu.
Amesema iwapo jamii itazidi kuhamasika kujifunza lugha hiyo itasaidia katika kuhakikisha ushiriki na ushirikishwaji wa watu hao unapatikana kwenye nyanja mbalimbali za kimaendeleo.
Amesema endapo jamii Itakua na uelewa wa lugha ya alama itasaidia katatua changamoto mbalimbali zinazolikabili kundi Hilo.
katika maadhimisho hayo kauli mbiu ya mwaka huu ungana kutetea haki za lugha ya alama.