Viongozi kaskazini unguja watakiwa kuwa na mashirikiano
14 June 2024, 10:04 am
Picha ya wakuu wa taasisi za mkoa wa kaskazini unguja wakiwa pamoja na mkuu wa mkoa huo Rashd Hadid Rashid (aliyeluwepo mbele) katika kikao maalum cha tathmini..
Uwepo na umoja na mshikamano kutwezesha kufanya harakati mbali mbali za kiserekali kwa ufanisi.
Na Abdul Sakaza.
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mh. Rashid Hadidi Rashid amewataka viongozi wa Mkoa huo kuendelea kutoa mashirikiano ya kila mwaka wakati wa mapokezi ya mwenge wa uhuru ndani ya Mkoa huo.
Amesema hayo katika kikao maalum chenye lengo la kutathmini Mwenge wa uhuru 2024 kilichofanyika ofisini kwake Mkokotoni mkoa wa kaskazini unguja.
Hadidi amesema amerizishwa na mashirikiano yaliotolewa na ofisi za Wakuu wa Wilaya kwa kuhakikisha wanafanikiwa katika kuupokea na kuutembeza mwenge wa uhuru katika miradi mbali mbali ya maendeleo ndani ya Mkoa huo.
Hata hivyo amekishukuru Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuonyesha jitihada zake kwa kamati ya ulizi na usalama pamoja na Serekali Ya Mkoa huo katika kufanikisha zoezi la kukimbiza Mwenge wa uhuru 2024.
Mwenge wa uhuru 2024 katika Mkoa wa Kaskazini Unguja ulipokelewa tarehe 20/05/2024 katika skuli ya maandalizi ya kiislamu mfenesini ukitokea mkoa wa mjini magharibi na tarehe 22 /05/2024 ulikabidhiwa Mkoa wa Kusini Unguja katika skuli ya msingi kilombero ili kuendelea na mbio zake.