Tumbatu FM

Kampeni za uchaguzi wa Mabaraza ya vijana Zanzibar zimeanza leo rasmin

19 February 2026, 10:50 am

Picha ya wagombea wa nafasi mbali mbali za uongozi kwenye uchaguzi wa baraza la vijana Shehia ya Tumbatu Uvivini wakiwa katika uzinduzi wa kampeni. Picha na Juma Haji .

kwa kuwa uchaguzi huu unahusu kundi la vijana pekee hakikisheni mnawafikia vijana hasa wenye kura ili kurahisisha kampeni kwa kuwahusisha walengwa zaidi”.

Na Juma Haji

Viongozi waliojitokeza kungombania nafasi za uongozi kwa mabaraza ya vijana Zanzibar unaotarajiwa kufanyika february 21 mwaka huu wametakiwa kuendesha kampeni kwa wanachama wa mabaraza ili kujenga ushawishi zaidi wa ushindi wao.

Akizindua kampeni za mabaraza ya vijana kwa shehia ya Tumbatu Uvivini katika ukumbi wa Almadrasat –Swabirina  ya Tumbatu Mkoa wa kaskazini Unguja mgeni rasmin katika hafla hiyo ambae pia ni sheha mshtahafu wa shehia ya Tumbau Uvivini Ndugu Hassan Mwadini Haji amesema wagombea wajipange kuwafikia vijana waliopo katika orodha ya wapiga kura kwani ndio wenye maamuazi ya mwisho ya kuwachagua.

Amesema hatua hiyo itapunguza changamoto za wagombea vijana kudharauliwa na kuvunjwa moyo na baadhi ya wanajamii wasiowapelendea mema vijana.

Akitoa nasaha kwa vijana amewataka viongozi watakaochaguliwa  kuimarisha umoja na mshikamano kwa wanachama na viongozi ili iwe rahisi kupanga mipango na kuitekeleza

Sauti ya sheha wa shehia mstahafu wa shehia ya Tumbatu Uvivini Ndugu Hassan Mwadini Haji

Akitoa ufafanuzi kwa wanachama juu ya maswala mbali mbali yaliyoulizwa mwenyekiti wa baraza la vijana shehia ya Tumbatu Uvivini Ali Bakili Sueaiman amewataka vijana watakaoshindwa kwenye uchaguzi kuunga mkono viongozi watakaochaguliwa ili kuongeza kasi ya utendaji wa shehia zao.

Amesema kukosa fursa hio vijana wajiandae kwenye fursa nyengine zitakazojitokeza kwenye utendaji wa ndani wa mabaraza yao.

Nae katibu wa baraza la vijana shehia ya uvivini Khamis Foum Khamis amesema wataitumia fursa ya uchaguzi kama ngazi pekee ya kufaidika na malengo ya serikali yaliowekwa kwa vijana kupitia mabara za ya vijana.

Sauti ya katibu wa baraza la vijana Khamis Foum Khamis

Hadi sasa Vijana waliojitokeza kuchukua fomu za kugombania nafasi za uongozi kwa shehia ya Tumbatu uvivini 18 kati yao wanawake 7, wanaume 11