Tumbatu FM
Tumbatu FM
27 October 2025, 12:24 pm

Ni wanachama wa umja wa watu wenye ulemavu Wilaya ya kaskazini “A” Unguja wakipatiwa mafunzo ya elimu ya mpiga kura Mkwajuni Wilaya ya kaskazini A:
“Jamii ijitokeze kuwasaidia watu wenye ulemavu kwa kuwafikisha kwenye vituo vya kupigia kura ili wa weze kupiga kura mapema na kurudi majumbani”
Na Juma Haji
Watu wenye ulemavu Zanzibar wameaswa kutokuwa chanzo cha uvunjifu wa amani katika uchaguzi wa mkuu wa Tanania utakaofanyika juma tano ya tarehe October 29 Mwezi huu.
Akifungua mafunzo maalum ya utoaji wa elimu ya mpiga kura kwa watu wenye ulemavu huko mkwajuni Wilaya ya kaskazini A” Unguja mwenyekiti wa Jumuiya ya watu wenye ulemavu Wilaya ya kaskazini A” Maulidi Juma Mwadini amesema watu wenye ulemavu wanapaswa kutoshawishika kuungana na watu wenye nia ovu ya kuchochea uvunjifu wa amani kwenye vituo wakati wa zoezi la upigaji wa kura.
Amesema njia nzuri za kujiepusha na changamoto za uchaguzi kwa watu wenye ulemavu ni kufuata taratibu walizoelekezwa kupitia mafunzo hayo zinazowataka kufika vituoni mapema ili wawahi kupiga kura mapema na kurudi majumbani.
Kiongozi huyo ametumia jukwaa hilo kuziomba taasisi zinazoendesha shughuli zake ndani ya mkoa wa kaskazini Unguja kuwahusisha watu wenye ulemavu ili na wawo wapate uelewa wa maswala mbali mbali yanayotokea kwenye Nchi.
Amesema taasisi hizo zinapaswa kuiga mfano wa taasisi zinazotoa elimu ya mpiga kura mwaka huu ikiwemo Shirika la Action AID na Jumuiya ya vija na elimu Mkoa wa kaskazini Unguja kwa kuamua kufikisha elimu hiyo kwa makundi yote katika jamii likiwemo kundi la watu wenye ulemavu.
Akitoa maada kwenye mafunzo hayo mkufunzi kutoka Shirika la Action Aid Tanzania ambae pia ni Mkurugenzi wa Jumuiya ya elimu ya Vijana Mkoa wa kaskazini Unguja Ndugu Mbarouk Maalumu Mohamed amewataka wananchi kutumia siku zilizobakia kuhakiki majina yao kwenye vituo walivyojiandikishia ili waweze kujua mahali wanastahiki kupiga kura kabla ya siku ya kura kufika
Amesema hatua hiyo itawapa uhakika wa kupiga kura nakuwapunguzia Usumbufu wa kutafuta taarifa hizo na hivyo kulazimika kutumia muda mwingi wakiwa vituoni mwa kura.
Wakichangia maada washiriki wa mafuno hayo akiwemo Bi Mwajuma Suleima na Bw Hassan Sulaiman Hassan wameshukuru kupatiwa mafunzo yayo na kuahidi kuwa mawakala kwa wenzao waliopo majumbani.
Mafunzo hayo ni ya siku moja yameandaliwa na Shirika la Action aid Tanzania kwa kushirikiana na Global Platform Tanzania chini ya usimamizi wa Tume huru ya taifa ya uchaguzi Nchini Tanzania (INEC)