Tumbatu FM
Tumbatu FM
20 July 2025, 10:35 am

“Ikiwa wahariri watasimamia vyema majukumu yao watasaidia kuondosha taarifa zinazopelekea migongano ndani ya jamii”
Na Juma Haji.
Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Dkt. Khalid Salum Mohhamed amewataka wahariri wa vyombo vya habari kuwa waangalifu juu ya maudhui wanayochapisha ili kuiepusha jamii na mifarakano.
Akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari juu ya ulinzi wa taarifa binafsi yaliyofanyika katika ukumbi wa BOT Kinazini mjini Zanzibar amesema ili taarifa iepukane na upotoshaji kwa mtumiaji ni lazima vyombo vya habari kukagua taarifa na madhara yake kabla ya kuchapishwa kwa umma.
Amesema kulingana na maendeleo ya sayansi na tekinologia kadri taarifa inavyosambaa kwa kasi ndivyo invyopokelewa bila kujali madhara yanayoweza kutokea kwa watumiaji wa taarifa hiyo.
Akitoa nasaha kwa waandisihi wa Habari walioshiriki mafunzo hayo Mkurugenzi mkuu wa Tume ya taifa ya ulinzi wa taarifa “PDPC” Dr Emmanuel L. Mkilia amewataka waandishi wa habari kujenga utamaduni wa kujifunza sheria za ulinzi wa taarifa zilipo nchini ili kuepuka migogoro ya kisheria ambayo inaweza kuathiri weledi wa kazi ya habari.
Awali akimkaribisha mgeni rasmin naibu katibu mkuu Wizara ya ujenzi na uchukuzi Bi Hawa Ibrahim amesema mafunzo hayo yamekuja wakati muwafaka na yatawasaidia waandishi wa habari kuimarisha mifumo ya ulizi wa taarifa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu na baada ya uchaguzi.
Amesema moja yajukumu la waandishi wa habari kwa sasa ni kuelimisha wananchi juu hatua kubwa za maendeleo zilizofikiwa ili Nchi iendeelee kubakia katika hali ya amani na utulivu.
Mafunzo hayo ya siku moja ya ulinzi wa taarifa binafsi yamewashirikisha waandishi wa habari, wahariri na maafisa habari wa Zanzibar yameandaliwa na Tume ya taifa ya ulinzi wa taarifa kwa kushirikiana na Clabu ya waandishi ya Zanzibar ZPC.