Tumbatu FM

SMZ yapinga ajira za utotoni

12 June 2025, 9:00 pm

Picha ya waziri wa nchi Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Sharif Ali Sharif. Picha na Vuai Juma

Ipo haja ya kuiunga mkono Serikali katika mapambano dhidi ya ajira za utotoni ili kuwapa watoto haki zao za kimsingi

Na Vuai Juma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Mhe, Shariff Ali Shariff ameitaka jamii na Taasisi mbali mbali nchini kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kutoa mashirikiano  ili kufikia lengo la kumaliza ajira za watoto.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari huko Ofisini kwake Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi B’ kuhusiana na maadhimisho ya siku ya kupinga ajira za watoto duniani amesema kuwa katika kuendelea na mapambano dhidi ya ajira za watoto Serikali imeweka mikakati madhubuti kukemea vitendo hivyo.

Aidha amefahamisha kuwa Zanzibar ni sehemu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imeridhia mikataba mbali mbali ya shirika la kazi Duniani, ambapo miongoni mwa mikataba hiyo ni mkataba nambari 138 wa mwaka 1973 unaohusu umri wa chini wa kuajiriwa na mkataba 182 wa mwaka 1999 inasisitiza kupiga marufuku na kuondoa kabisa aina mbaya zaidi ya ajira za watoto.

Waziri Shariff amefahamisha kuwa Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi mwanachama wa Shirika la Kazi Duniani (ILO), bado inakabiliwa na tatizo la ajira za watoto, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Mtakwimu Mkuuu wa Serikali kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mtakwimu Novemba 2024 zinaonesha kuwa watoto milioni 5.1 wamo katika ajira za watoto.

Amefafanua kuwa watoto milioni 160 Ulimwenguni wamo kwenye ajira za watoto ambapo kwa Tanzania Bara watoto kati ya miaka 5-17 sawa na asilimia 25.3 wanafanya kazi, asilimia 25.5 wamo kwenye ajira za watoto na asilimia 24.3 wanafanya kazi hatarishi na kwa upande wa Zanzibar watoto wenye miaka kati ya 5-17 asilimia 7.6 ya watoto wanaofanya kazi, asilimia 7.5  walio kwenye ajira za watoto na asilimia 7.4 wanafanya kazi hatarishi.

Sauti ya waziri wa wa nchi Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Sharif Ali Sharif

Aidha ameeleza kuwa mbali na hayo maafisa kutoka Zanzibar walikwenda Tanzania bara kujadili mkakati wa kuweka dawati katika bandari ya Dar es salam ili kupambana na kadhia hiyo ya kupinga ajira za watoto nchini.

Maadhimisho ya Siku ya Kupinga ajira za watoto duniani hufanyika kila ifikapo June 12 ambapo Kaulimbiu ya mwaka huu.