Tumbatu FM

UWZ yaanza  ziara za kuitambulisha bodi tendaji mpya

11 May 2025, 10:37 am

Pichani ya wajumbe ya umoja wa watu wenye ulemafu Zanzibar wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya umoja huo Bw Abdulwakil Haji Hafidh na wapili yake ni katibu Bodi hiyo Bwana Yahya Hamed Saidi wakiwa katika kikao huko huko Gamba Wilaya ya kaskazini “A” Unguja. Picha na Juma Haji

Na Juma Haji

“Tutafika kila Wilaya kuonana na wanachama wa jumuiya ya watu wenye ulemavu Zanzibar na kuwasikiliza ili tuwende sambamba nao kwenye uendeshaji wa jumuiya”

Na Juma Haji

Wajumbe wa Bodi tendaji ya Umoja wa watu wenye ulemavu Zanzibar wameaza  ziara za kujitambulisha kwa walengwa wao katika Wilaya zote za Unguja na Pemba.

Wakiwa kwenye ziara huko Gamba Wilaya ya kaskazini “a” Unguja wamesema lengo la ziara hizo ni kujitambulisha na kusikiliza mawazo ya walengwa ikiwa ni njia moja wapo ya kutafuta ushauri na mawazo yatakayosaidia kuboresha mipango ya taasisi hiyo katika muhula wao wa uongozi.

Akiwasilisha maada katika mkutano huo Mwenyekiti wa Bodi ya Umoja wa watu wenye ulemavu zanzibar (UWZ ) Bw Abdulwakil Haji Hafidh amewataka wajumbe wa kamati za Wilaya na washiriki wengine wa mikutano hiyo kutumia fursa hiyo vizuri   ili lengo la ziara hiyo liweze kufikiwa.

Amesema katika kipindi chote tokea kuazishwa kwa umoja wa watu wenye ulemavu Zanzibar UWZ mwaka 1985 umoja huo umeongozwa na viongozi tofauti na mambo mengi ya kimaendeleo yamefanyika ikiwa ni pamoja na miradi na matukio ya utatuzi wa changamoto za watu wenye ulemavu.

Picha ya yashiriki wa mkutano wa watendaji na viongozi wa bodi ya watu wenye ulemavu Zanzibar

Picha na Juma Haji

“Ikiwa kutaanzishwa mfumo wa pencheni kwa watu wenye ulemavu kutasaidia kuwaondolea changamoto za kimaisha.

Wakichangia maada kwenye mkutano huo baadhi ya washiriki akiwemo Bw Ali Khamisi Makame Na Bi Ulaya Khamis Juma ameomeiomba Bodi kuendelea kufuatilia wazo la kuazishwa pencheni ya watu wenye ulemavu Serekalini, kuendeleza mradi wa CBR pamoja na mkakati wa kutoa vifaa kwa watu wenye ulemavu kila baada ya muda.

Nae Mwenyekiti wa kamati ya Uwz Wilaya ya kaskazini “A” Bw Maulidi Juma Mwadini amewapongeza viongozi hao kwa kufika kwa wanachi na kuahidi kuwapa ushirikiano katika uongozi wake.

Ziara za Bodi tendaji ya Uwz kwa walengwa wake zimeaaza katika Wilaya za Unguja na zitaendelea kwenye Wilaya za Pemba.