Miaka 10 ya Tumbatu Fm, wenye ulemavu wathaminiwe
16 November 2023, 3:13 pm
Radio ya jamii Tumbatu inaadhimisha miaka kumi tangu kuanzishwa kwake ambapo maadhimisho hayo yanaambatana na kufanya matendo ya huruma kwa jamii hasa wenye mahitaji maalum.
Na Mwanahawa Hassan.
Jamii imetakiwa kuishi vizuri na watu wenye ulemavu na kuwapatia mahitaji yao ya msingi.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Watu Wenye Ulemavu wilaya ya Kaskazini A Unguja Khamis Rashid Khamis wakati wa zoezi la ugawaji wa vifaa visaidizi kwa watu hao ikiwa ni shamrashamra zakuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu na maadhimisho ya miaka kumi(10) tangu kuanzishwa kwa kituo cha Redio jamii Tumbatu.
Amesema lengo la kupatiwa hivyo vifaa ni kuhakikisha wanafanya harakati zao bila ya usumbufu wowote hivyo amewataka wazazi na walezi kuvitunza vifaa walivyopatiwa watoto wao ili kufikiwa lengo la msaada huo.
“Ni lazima tuwajali watu wenye ulemavu ili kwani nao wana haki sawa na kama watu wengine”
Sauti ya Khamis Rashid Afisa wa watu wenye ulemavu wilaya ya Kaskazini Unguja.
“Tukiwasaidia watu wenye ulemavu tutwaweza kuwaondoshea changamoto mbalimbali”
Picha Na Latifa Ali.
Kwa upande wake katibu wa Jumuiya ya Watu wenye Ulemavu wilaya ya Kaskazini A Bi: Ulaya Khamis Juma ameishukuru taasisi ya UWT wilaya ya Kaskazini “A” kupitia Chama Cha Mapinduzi, Baraza la watu wenye ulemavu taifa kwa kushirikiana na radio jamii Tumbatu kwa msaada walioutoa.
Aidha ameishukuru kwa dhati Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwatambua watu wenye ulemavu kwa kuwawekea baraza la watu wenye ulemavu na kuweza kujitambua jambo ambalo linawapa matumaini katika kuzitatua changamoto zao.
Pichani ni Katibu wa Jumuiya ya Watu wenye Ulemavu wilaya ya Kaskazini A (aliyeshikilia kiti.) Picha naLatifa Ali.
Kwa upande wake sheha wa shehia ya Nungwi Banda Kuu bwana Ali Khamis Haji amewaomba watu wanaotafuta misaada kwa ajili ya kuwasaidia watu hao kufikisha misaada sehemu husika kwani wapo watu wenye tabia ya kujinufaisha na misaada hiyo hata kama hawana ulemavu wowote.
Sauti ya sheha wa shehia ya Nungwi Banda Kuu
Nae Bwana Machano haji kutoka Shehia ya nungwi banda kuu ambaye ni miongoni mwa wanufaika wa msada huo ametoa shukran kwa msada waliopatiwa utakaowawezesha kufanya harakati zao.
Sauti ya Bwana Machano Haji Ambaye ni mnufaika wa msada huo.
Radio ya jamii Tumbatu inaadhimisha miaka kumi tangu kuanzishwa kwake ambapo maadhimisho hayo yanaambatana na kufanya matendo ya huruma kwa jamii hasa wenye mahitaji maalum.