Wakulima Kibokwa watakiwa kupisha uwekezaji
12 November 2023, 12:18 pm
Picha ya waziri wakilimo na umwagiliaji Shamata Shame (aliye nyoosha kidole)akiwa katika kikao na wakulima wa bonde la mpunga kibokwa. Na Abdul – Sakaza.
“Ushirikishwaji kati ya serekali na wakulima katika harakati za kimaendeleo kutasaidia kutatua changamoto mbalimbali hasa linapokuja suala la uwekezaji”
Na Abdul – Sakaza.
Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo wa Zanzibar, Mhe. Shamata Shaame Khamis, amewetaka wakulilima wa bonde la mpunga Kibokwa eneo la Ukweli Bora shehia ya Kinyasini kuwapisha wawekezaji katika maeneo hayo ili kuongeza kasi ya upatikanaji wa chakula nchini.
Akizungumza na wakulima wa eneo hilo Mhe. Shamata amesema Kaskazini Unguja wamepata fursa ya kipekee kutoka kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hivyo ikiwa wataruhusu wawekezaji kuwekeza katika mabonde hayo ya mpunga kutasadia kuongeza huduma ya chakula kwa wananchi na kupunguza ukali wa maisha .
Picha za wakulima wa mpunga maeneo ya kibokwa shehia ya mfenesini. Na Abdul – Sakaza.
Kwa upande wao wakulima wa bonde hilo la mpunga wameiomba serikali kuandaa miundombinu rafiki kwa wakulima hao ikiwemo kuwatafutia sehemu mbadala ambazo zitawasadia kuendeleza kilimo chao.