Wanahabari watakiwa kuongeza taaluma zaidi
4 September 2023, 4:55 pm
Ikiwa wandishi wa habari watajenga tabia ya kujifunza zaidi kuhusu madhara ya upungufu wa damu hasa kwa wananwake na wasichana wataweza kuandaa vipindi vilivyo bora na ambavyo vitatoa masada mkubwa kwa jamii juu ya kukabiliana na tatizo hilo.
Na Juma Haji.
Naibu katibu mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mwanakhamisi Ame Ameir amewataka wandishi wa habari kujielimisha kabla ya kuandaa vipindi ili kuifikishia jamii taarifa zilizo sahihi.
Akizungumza na waandishi wa habari huko skuli ya Kiembe Samaki katika mafunzo maalum kwenye program ya kukabiliana na upungufu wa damu kwa wasichana amesema iwapo waandishi watakuwa na uelewa wa kutosha juu ya taarifa wanazozitoa itaondoa maswali na hofu kwa jamii katika kufuatilia taarifa hiyo.
Amewataka waandishi wa habari kuwatumia watendaji wa wizara ya afya na wizara ya elimu na mafunzi ya Amali wanaosimamia program hiyo katika kuongeza uelewa kwenye campeni ya kukabiliana na upungufu wa damu kwa wasichana Zanzibar.
Akitoa nasaha mkufunzi wa mafunzo hayo Bi Asha Hassan Salmin amewataka wanahabari kuyafanyia kazi mafunzo waliyopatiwa kwa kuandaa program nzuri na zenye kufikisha ujumbe kwa jamii.