Ruangwa FM

Kilele cha maadhimisho miaka 63 ya Uhuru yafanyika Ruangwa

8 December 2024, 7:24 pm

DC Moyo akizungumza miaka 63 ya uhuru Tanzania Bara. (picha na Magoma.)

Na Mwanne Jumaah

Maadhimisho ya  miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara yamefanyika leo, tarehe 8 Desemba 2024, katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi,Sherehe hizo zimefanyika katika viwanja vya Likangara, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, ndugu Mohammed Moyo.

Akizungumzia maendeo ya wilaya ya ruangwa mkuu wa wilaya ya nachingwea Mohamed Moyo ambae alikua mgeni rasmi, alieleza kuwa maendeleo yanayoonekana sasa katika Wilaya ya Ruangwa na taifa kwa ujumla ni matokeo ya uhuru, na kwamba maendeleo haya yanaendelea kuchochewa na uongozi madhubuti na ushirikishwaji wa wananchi.

kwa upande wake Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ruangwa, Komredi Abbas Makweta, alieleza jinsi wakoloni walivyokuwa wakitawala Tanganyika na kuzuiya maendeleo ya nchi, na Amesisitiza kuwa kupitia uhuru wa nchi, maendeleo makubwa yameweza kupatikana.

Maadhimisho haya ambayo hufanyika kila mwaka kulingana na agizo la mh dkt Samia suluhu Hassan la ufanyaji wa maadhimisho hayo yameambatana na mashindano ya michezo mbalimbali huku washindi wakipata zawadi mbali mbali ,usafi wa mazingira pamoja na upandaji miti katika hospitali na magereza wilayani hapa .

Ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Maadhimisho ya miaka 63 ya uhuru Tanzania Bara Uongozi Madhubuti na Ushirikishwaji wa Wananchi ni Msingi wa Maendeleo Yetu.”