Chuo kikuu cha Dar es salaam kutoa Shahada ya pili na ya tatu ya kilimo Ruangwa
31 January 2023, 12:06 pm
Ujenzi wa chuo kikuu cha Dar es salaamu tawi la Ruangwa kitakachotoa Shahada ya pili na ya tatu katika ngazi ya kilimo unatarajia kuanza Juni 2023.
Na Loveness Daniel.
Ujenzi wa chuo kikuu cha kilimo kupitia chuo kikuu cha dar es salaam tawi la Ruangwa makao makuu yake yakiwa lindi Ngongo kwa mchepuo wa kilimo unatarajia kuanza jun 2023 ili kuanza kutoa elimu kwa ngazi ya shahada ya pili na ya tatu.
Hayo yamebainishwa leo na mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam ambae pia ni raisi mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete January 2023 alipotembelea eneo linalotarajiwa kujengwa kwa tawi hilo la chuo eneo la kitandi wilayani Ruangwa Mkoani lindi.
Dkt Kikwete amesema chuo makao makuu yake yatakua mkoani lindi eneo la ngongo ambapo watatoa shahada ya kwanza na eneo la nanambye kutakua na mashamba lakini tawi la Ruangwa Litakua Linatoa ya shahada ya pili na ya tatu ambapo ameitaka halimashauri kumalizana na wamiliki wa aridhi hiyo ili waanze ujenzi bila ya migogoro.
“Malizaneni na wakulima mapema sisi hatutaki kukuta migogoro ili tuanze ujenzi wetu mapema haya mashamba ya watu msipomalizana nao inaweza kuleta migogoro malizaneni nao mapema” Alisema Dkt. Mrisho Kikwete.
“Malizaneni na wakulima mapema sisi hatutaki kukuta migogoro ili tuanze ujenzi wetu mapema haya mashamba ya watu msipomalizana nao inaweza kuleta migogoro malizaneni nao mapema” Alisema Dkt. Mrisho Kikwete.
Awali akisoma taarifa ya eneo lilitengwa Afisa Aridhi Peter Hanjay kwa niaba ya mkurugenzi amesema Zaidi ya ekari 405 zimetolewa na halimashauri ya wilaya ya ruangwa kwa ajili ya ujenzi wa tawi la chuo hicho ambapo kukamilika kwa chuo hicho kutasaidia kuinua uchumi na fursa za kielimu wilayani ruangwa.
Aidha Hanjay amesema tayari hatua za awali za utekelezaji zimefanyika kama kukutana na wamiliki wa mashamba hao wale wa asili na kuzungumza nao pia wapo tayari kwa tayari hatua za awali za ajili ya kutoa aridhi na pia wamefanya tathimini na upimaji hivyo hivi karibuni watakamilisha hati za malipo kwa wamiliki kupisha aridhi kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi.