Ruangwa FM
Ruangwa FM
27 June 2025, 1:24 pm

Na khadja Omari
Mkuu wa Wilaya ya Lindi Bi Victoria Mwanziva, amesema Serikali ya awamu ya sita inatambua na itaendelea kufanya jitihada mbalimbali za kuwawezesha wajane kama ilivyo kwa makundi mengine, kuwapa stahiki zao ikiwa pamoja na utatuzi wa matatizo yao.
Akizungumza Kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Katibu tawala uchumi na uzalishaji kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo Bwn. Mwijuma Mkungu wakati wa maadhimisho ya siku ya wajane kimataifa, iliyofanyika kwa Ngazi ya Mkoa katika Manispaa ya Lindi amesema serikali inatambua umuhimu wa kundi hilo kwa ustawi wa Maendeleo ya jamii.
Ameongeza kuwa Serikali bado inaendelea kuhamasisha Jamii kuachana na Mila na desturi zenye madhara kama kunyang’anya Mali za wajane kuozesha watoto wa kike Katika umri mdogo kutakasa na kurithi wajane pamoja na Mila zote zinazoweza kumdhoofisha mwanamke .
Awali akisoma risala ya chama cha wajane mkoa wa Lindi Bi. Rehema Shambi amesema lengo la kuanzishwa chama hicho ni kuwaunganisha wajane na kubadilishana uzoefu ili kutunza na kuboresha familia zao.
kaulimbiu ya siku ya wajane kimataifa ni “Tuimarishe fursa za kiuchumi kuchochea Maendeleo ya wajane”.