Ruangwa FM
Ruangwa FM
12 June 2025, 3:05 pm

Na Loveness Josefu
“Wananchi tuimarishe afya zetu kwa kufanya mazoezi na kuzingatia ulaji unaofaa”
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa mkoa Wa Lindi Mhe. Zainabu Telack leo 12 Jun 2025 katika mbio za ridhaa zilizofanyika asubuhi mapema kwa kuianza siku ya pili ya maonesho ya madini na fursa za uwekezaji Mkoani Lindi.
RC Telack amesema tuzingatie ulaji unaofaa kwa kudumisha afya zetu ili kuweza kuimarisha afya zetu ambazo ndio nguzo yetu.
Aidha Mkuu wa wilaya ya Ruangwa Mhe.Hassan Ngoma amepongeza vijana kwa kushiriki mbio za marathon pamoja na viongozi kuonesha mfano mkubwa.

”vijana tuna cha kujifunza hapa mkuu wa mkoa ameshiriki km5 zote kwa mbio hizi na umri wake kweli umri ni namba tu tushiriki mazoezi”amesema DC Ngoma.