Mratibu wa malaria wilaya ya Ruangwa akitoa elimu
Ruangwa FM

Wadau wa Mradi wa Dhibiti Malaria (PMI) wamaliza ziara ya elimu wilayani Ruangwa

3 December 2024, 7:57 pm

wananchi wakipata elimu dhidi ya ugonjwa wa malaria. (picha na Mwanne Jumaah)

Na Mwanne Jumaah

Wadau wa Mradi wa Dhibiti Malaria (PMI) wamemaliza ziara ya kutoa elimu dhidi ya ugonjwa wa malaria katika kata za Mandarawe, Malolo, Chienjele, Mnacho, na Nandagala zilizopo wilayani Ruangwa, mkoani Lindi, jana, tarehe 02 Desemba 2024,Ziara hii ilikuwa ni sehemu ya juhudi zaserikali katika  kuelimisha jamii kuhusu hatari za malaria na njia bora za kujikinga na ugonjwa huo.

Ziara hii ya elimu ilianza katika kata za Mbwemkulu, Mandawa, Chunyu, Mbekenyera, na Narungombe, ambapo wananchi walipata taarifa muhimu kuhusu malaria.

Aidha Mratibu wa Malaria wilaya ya Ruangwa, Dkt. Ezekia Ambikile, alitoa ufafanuzi wa kina kuhusu ugonjwa wa malaria, dalili zake, na hatua zinazopaswa kuchukuliwa na wagonjwa. Huku , Dkt. Ambikile akisisitiza umuhimu wa kupata vipimo kutoka vituo vya afya kabla ya kutumia dawa za malaria, akisema kuwa sio kila homa inahusisha malaria.

Ziara hiyo ilifanyika kwa awamu ya pili ikiwa na mtindo wa maonesho kwa vitendo yakihusisha burudani na maigizo yenye kuisogeza jamii karibu na ni muendelezo wa programu ya kudhibiti malaria nchini, hasa kwa watoto wachanga na wanawake wajawazito, na inaimarisha juhudi za serikali katika kupambana na ugonjwa huo wa malaria ambao umekua na athari katika jamii.