Ruangwa FM

DC Ruangwa: Hatutaangalia chama, ukiibua taharuki sheria itafuata mkondo wake

8 November 2024, 10:44 pm

Madiwani wakiwa katika baraza la madiwani.

Mkuu wa wilaya ya Ruangwa Hassan Ngoma amewataka madiwani , Viongozi mbali mbali wa vyama vya siasa kutoibua taharuki yeyote itakayovuruga amani kipindi cha uchaguzi wa serikali za mtaa bali wawe sehemu ya kuleta amani katika jamii na kuleta suluhisho kwenye migogoro ili kufanya uchaguzi wa haki na Salama.

DC Ngoma ameyasema hayo jana katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa halimashaur ya wilaya ya Ruangwa.

DC Ngoma amewasisitiza viongozi hao kua uchaguzi ni wa siku moja hivyo viongozi waepuke kutengeneza uadui utakaodumu katika jamii kwa kuumiza watu, kutengeneza migawanyiko na chuki katika jamii na kusema kama serkali ya wilaya haitavumilia kiongozi wa namna hiyo.

Akizungumza katika baraza hilo katibu wa waziri mkuu Jimboni Comredi Ramadhan Matola amesisitiza viongozi kutumia nafasi zao kuhamasisha wananchi kupiga kura.

Aidha kwa upande wake Mwenyekiti Wa ACT wilaya ya Ruangwa ndg Bakari Kungoni amesisitiza umoja ili kuweza kuletea wananchi mabadiliko na Ruangwa kua wilaya ya kuigwa huku Mwenyekiti wa CUF ndg Liwikila Mohamed (Obama) akisisitiza wananchi kupatiwa elimu ya demokrasia.