Ruangwa FM

Kifungo cha maisha kwa kubaka mtoto wa miaka 4 Ruangwa

23 August 2024, 9:25 am

Mahakama ya Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi imemhukumu kifungo cha maisha jela kijana Issa Mushizo (23) mkazi wa Nandanga wilayani Ruangwa kwa kosa la kubaka mtoto mwenye umri wa miaka minn (jina limehifadhiwa).

Mtuhumiwa alitenda kosa hilo 10 Januari 2024 na kukamatwa 11 Januari 2024 kisha kufikishwa mahakamani na kusomewa shtaka lake linalomkabili.

Hata hivyo mtuhumiwa alikana mashtaka hadi pale ushahidi ulipomtia hatiani.