Elimu maalum Namakonde wapewa vitanda, magodoro waishi shule
4 August 2023, 1:02 pm
Wanafunzi wenye ulemavu wanaosoma shule ya Msingi Namakonde wilayani Ruangwa mkoani Lindi, wamepatiwa msaada wa magodoro na vitanda kutoka kampuni ya Uranex inayojihusha na uchumbaji wa madini ya kinywe (graphite) wilayani humo kwa ajili ya kutumia katika mabweni yaliojengwa na serikali ili kuwasaidia kuepuka changamoto ya usafiri miongoni mwao na badala yake waweze kulala papo hapo shuleni.
Hatua hiyo inakuja kufuatia kukamilika kwa ujenzi wa mabweni mawili mahususi kwa Watoto wenye ulemavu shuleni hapo yaliojengwa na serikali kupitia miradi ya Lipa kulingana na matokeo GPE II – LANES Pamoja na ule mradi wa Uvico 19.
Awali akipokea msaada huo Mapema 3 Agost, 2023 kaimua mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa Ernest Haule,ameeleza msaada huo kuwa umefika katika wakati muafaka na kwamba serikali iliwasaidia ujenzi wa mabweni lakini vitanda na magodoro havikuwapo huku meneja wa kampuni ya Uranex Mhandisi wa Isaac Mamboleo alisema kuwa wamekabidhi vitanda 25 na magodoro 50 ikiwa shemu ya mchango wao kwa jamii hasa katika kuichangia sekta ya elimu.
vifaa hivi vimekuja muda muafaka kwa sabau serikali ilitujegea mabweni lakini vitanda na magododro hayakuwepo kwahiy sisi tunashukuru sana. alisema Haule
Katika hatua hiyo walimu akiwamo Mwalimu Juma Chitime anefundisha wanafunzi hao alieleza kuwa Vifaa hivyo vitapunguza changmoto za usafiri miongoni mwa wanafunzi hao kwani wanapokaa shuleni hawatapata usumbufu wao n ahata wazazi wao huku wanafunzi nao akiwamo sumaiya Dadi na Aminata Ferooz wakieleza kutumaini kulala vizuri na kuwahi darasani.
Wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika shule ya msingi Namakonde ni 38 ambapo kati yao wasichana ni 21 na wavulana 17 wanaotegemewa kuanza kunufaika na kukaa shuleni hapo baada ya kukamilika kwa ujenzi wa mabweni yao na kupatikana kwa vitanda na magodoro.