Aga Khan Foundation yaja na mafunzo endelevu ya walimu kazini kukuza taaluma Ruangwa
18 May 2023, 7:41 pm
Kaimu mkurugenzi halmashauri ya wilaya ya Ruangwa ambaye pia ni afisa elimu msingi wilaya ya Ruangwa Mwl. George Mbesigwa amewataka walimu kutumia mafunzo yaliyoletwa na Aga Khan foundation wilaya ya Ruangwa kupitia MEWAKA kuyatumia vizuri katika kukuza taaluma mashuleni kwa lengo la ufundishaji na ujifunzaji mashuleni na katika vituo vya mafunzo kwa walimu.
Hayo ameyasema na Mwl. Mbesigwa wakati akifungua mafunzo hayo yanayofanyika wilaya ya Ruangwa kwa walimu wakuu wa shule za msingi , walimu mahiri shule za msingi, pamoja na walimu wezeshi ikiwa mafunzo hayo yanategemewa kunufaisha shule zote 89 za msingi wilayani Ruangwa. Mafunzo hayo yanafanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Ruangwa.
Aidha mratibu wa miradi kutoka Aga Khan Foundation mkoa wa Lindi Mwl. Shabani Sammatha amesema kupitia mradi wa Foundation follen unasaidia katika mafunzo endelevu ya walimu kazini (MEWAKA ) wanashirikiana na halimashauri ya wilaya ya Ruangwa ili kuwapatia waalimu taaluma na utaalamu Zaidi ambao utaenda kuboresha Zaidi hali ya taaluma wilayani hapa.
Gervas Antony ni Mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka chuo cha ualimu Mtwara amesema mafunzo hayo ni ya uwezeshaji rika ambayo wanapewa waalimu kwa kuendelea kujifunza wakiwa mashuleni kwa lengo la kuwafikia wanafunzi na kuwatengenezea ubora Zaidi katika ufundishaji na ujifunzaji wao.
‘’Tunawasaidia waalimu ili waweze kusaidiana wenyewe kwa wenyewe na kubadilishana uwezo wakiwa katika vituo vyao vya kazi pamoja na kusaidiana katika changamoto wanazokutananazo kwani mwalimu akiwa bora katika taaluma ufaulu utakua vizuri kwa wanafunzi’’amesema mwl Gervas
Baadhi ya waalimu walioshiriki mafunzo hayo wameeleza namna mafunzo hayo yalivyo na umuhimu katika kudumisha taaluma zao wakiwa shuleni.