Ruangwa FM

Ruangwa yapata milioni 965.9 kutekeleza ujenzi wa miundombinu elimu awali & msingi kupitia mradi wa boost.

8 May 2023, 6:48 pm

Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi imepokea 965,900,000/= Milioni mia tisa na sitini na tano na laki tisa, kutoka Serikali kuu kupitia mradi wa kuboresha upatikanaji wa fursa sawa katika ujifunzaji bora wa Elimu ya Awali na Msingi Tanzania Bara.

Kufuatia hatua hiyo mkuu wa wilaya ya Ruangwa Hassan Ngoma ameagiza mkurugenzi wa Halmashauri hiyo na watendaji kuhakikisha miradi inasimamiwa kwa mujibu wa sheria na utaratibu uliowekwa na kwa watakaokiuka hatua kali kuchuliwa dhidi yao.

Akizungumza Mapema mei 6, 2023katika kikao maalumu kilichohusisha wanakamati wanaosimamia utekelezaji wa mradi wa BOOST wilaya ya Ruangwa, mkuu wa wilaya hiyo Hassan Ngoma ameagiza kuwapo kwa nyaraka zote katika kila eneo mradi unapotekelezwa kwa mujibu wa muongozo na kusisitiza kuwa ni muhimu kila kinachofanyikaa katika mradi kiwekewe katika kumbukumbu.

Naagiza katika kila mradi kuwe na mafaili ya kuweka kumbukumbu za kila kinachofanyika manunuzi na kila kitu mimi nikija na timu yangu wengine watakagua jengo na wengine watavamia nyaraka ili kujiridhisha’ alisema Ngoma

Katika hatua hiyo pia Mhe,Ngoma amewataka watendaji kuwa mfano kujenga miradi yenye ubora huku mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo Frank Chonya akitangaza fursa kwa wananchi watakaoweza kufyatua Tofali.

kama kutakua na wafytuaji Tofali wenye uwezo wa kufyatua tofali zenye ubora sisi tutaruhu wao ndio watumike aktika kila eneo la mradi, kwahiyo vijana wajitokeze waonyeshe uwezo wao wapate kazi zitakazowaongezea kipato” alisema Chonya

Kwa upande wake Afisa elimu Awali na Msingi wilaya ya Ruangwa Mwl George Mbesigwe amesema kukamilika kwa miradi hiyo kutatatua changamoto ya miundombinu ambayo awali ilikua ikikabili baadhi ya maeneo huku Baadhi ya wananchi wakiwamo Glaciano Malibiche na Saidi Kauchumbe wakitoa angalizo la ukadiliaji sahihi wa mahitaji ya vifaa vya kujengea katika usimimazi wa miradi hiyo kutokana na uzoefu wa miradi iliyopita kuwapo kwa baadhi ya vifaa vilivyobaki ikiaminika ilitokana na ukadiliaji uliozidi mahitaji.

Mradi wa BOOST katika wilaya ya Ruangwa unategemewa kutekeleza ujenzi wa vumba vya madarasa 9, Matundu ya vyoo 12 pamoja na ujenzi wa shule 2 mpya zenye madarasa ya mondo mmoja mmoja.