kuelekea miaka 59 ya muungano Lindi yazindua siku ya upandaji miti kimkoa
20 April 2023, 7:46 pm
Na loveness Daniel
Kuelekea maadhimisho ya sikukuu ya miaka 59 muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambayo hufanyika April 26 kila mwaka Mkoa wa Lindi umezindua siku ya upandaji miti kimkoa ikiwa ni miongoni mwa utekelezaji wa agizo la Rais Samia Suluhu Hassan alilolitoa hivi karibuni ambapo aliagiza sherehe hizo kwa mwaka 2023 zifanyike kwa ngazi za mikoa.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo lililofanyika April 19 2023 katika shule ya Sekondari ya Wasichana Lindi Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mkuu wa Wilaya hiyo Shaibu Ndemanga ameagiza zoezi hilo la upandaji miti kuwa Endelevu katika taasisi zote serikali na watu binafsi na hasa uanzishaji wa bustani za miti ya matunda mashuleni.
Christopha Ngubiagai ni mkuu wa wilaya ya Kilwa ameeleza moja ya changamoto inayoathiri misitu katika wilaya hiyo na maeneo jirani ni uanzishwaji wa mashamba mapya ya ufuta huku afisa muhifadhi mwandamizi wakala wa misitu Tanzania TFS Lukas Sabida akieleza namna TFS inavyoshirikiana na na wadau wengine katika kutunza na kuhifadhi misitu.