RUNALI YAWANOA VIONGOZI VYAMA VYA MSINGI
Ruangwa FM

RUNALI yawanoa wajumbe wa vyama vya msingi

19 April 2023, 11:29 pm

Na Loveness Daniel

Chama kikuu cha ushirika RUNALI kinachojumuisha wilaya ya Ruangwa,Nachingwea na Liwale kimetoa mafunzo kwa wajumbe wa vyama vya msingi katika  jumla ya amcos 106 leo 19 April 2023 mafunzo hayo yamefanyika ghala la Runali  wilaya ya ruangwa.

Akizungumza dhumuni la mafunzo hayo manager  mkuu wa chama cha ushirika wa RUNALI Bi Jahida Hassan amesema kua lengo ni kuwajengea uwezo viongozi wa vyama vya msingi (makatibu wakuu wenyeviti na ma maneja wa vyama vya msingi),kwani mafunzo hayo yamelenga kuwafunza utawala bora,uandaaji,usimamizi na utunzaji wa nyaraka ili kupata hati safi.

‘’Tumeona tuwashirikishe COASCO,Takukuru,maafisa ushirika, maafisa kilimo ambao wametoa elimu ili kuhakikisha hawa viongozi wanaleta hati safi lakini pia kuanzisha miradi mipya na miradi ya uwekezaji na tunafanya hivi kuboresha na kuleta tija ya katika vyama vyetu kwakua ushirika ni biashara’’amesema Jahida hassan

‘’Tumeona tuwashirikishe COASCO,Takukuru,maafisa ushirika, maafisa kilimo ambao wametoa elimu ili kuhakikisha hawa viongozi wanaleta hati safi lakini pia kuanzisha miradi mipya na miradi ya uwekezaji na tunafanya hivi kuboresha na kuleta tija ya katika vyama vyetu kwakua ushirika ni biashara’’amesema Jahida hassan

sauti manager chama kikuu cha ushirika RUNALI

Aidha mkaguzi  kutoka COASCO Hansi kishiwa amesema  kupitia elimu aliyoitoa  itawasaidaia kwani baadhi  ya viongozi wa vyama vya ushirika imekua changamoto kuweka hali halisi ya thamani ya mali za vya ushirika katika taarifa zao  lakini pia  utunzaji wa  nyaraka za ushirika imekua ni changamoto ambayo inasababisha bodi zinazochaguliwa kushindwa kujua taarifa za bodi iliyopita hivyo amewataka kutunza taarifa katika nyaraka ili kupunguza migogoro katika ushirika.

sauti mkaguzi COASCO

Baadhi ya wajumbe katika vyama vya ushirika Ruangwa,Nachingwe na Liwale wameiomba runali kuwapatia mafunzo mara kwa mara lakini pia kuitumia elimu hiyo kuleta tija katika vyama vyao kwa kutatua migogoro kwa kuzingatia sharia pia kutunza nyaraka katika mifumo husika ili kupunguza migogoro ambayo imekua ikididimiza ushirika.

sauti wajumbe vyama vya msingi