Ruangwa FM

Kushindwa kumtunza mtoto ni kosa kisheria

30 January 2023, 7:32 am

Ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya sheria nchini, Mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi, imeendela na utaratibu wa kupita katika tarafa za wilaya hiyo ili kutoa elimu ya masula ya kisheria kwa wananchi.

Akizungumza na wananchi wa Tarafa ya mandawa wilayani humo januari 26 mwaka huu,Afisa wa jeshi la polisi kutoka Dawati la Jinsia Afande CPL Mpokigwa Mwamulangala, aamewaeleza wananchi wa tarafa hiyo kuwa ni kosa kisheria kwa wanaume waliokua na tabia za kuzaa na wenzi wao kisha kutokutoa huduma kwa Watoto jambo linalopelekea ongezeko la Watoto wasiokuwa na makazi maalumu.

Wananchi wakiwa katika mkutano wa kusikiliza msaada wa masuala ya kisheria, ofisi ya hakim mkazi mfawidh mahakama ya wilaya ya Ruangwa ilipowafikia wakazi wa Tarafa ya Mandawa.

Afande Mpoki amesema dawati la jinsia jeshi la polisi wilaya ya Ruangwa limekua likipokea malalamiko mengi hasa ya akina mama kulalamikia wazazi wenzao kutokuwapa huduma Watoto pindi wanapoachana.

Sauti ya Afande Mpokigwa Mwamulangala kutoka Dawati la jinsia Jeshi la Polisi Ruangwa.

Akisisitiza juu ya uwapo wa malalamiko kuachiwa Watoto na kuwalea peke yao kwa akina mama wilayani humo, Mwinyi Madi ambae ni afisa ustawi wa jamii anaepokea malalamiko ya wananchi kuhusu Malezi na changamoto mbali mbali za kifamilia, amekiri kuwapo kwa wimbi kubwa la wanawake wanaofika katika ofisi ya malalamiko wilayani humo ambapo wengi wao wanakabiliwa na changamoto ya kutokusaidiwa kuduma za maelezi kwa Watoto na wazazi wenzi wao.

“yaani pale ofisini kila siku ukifika kesi nyingi ni za akina mama kutosaidiwa huduma za malezi ya Watoto na wanaume waliozaa nao” alisema Mwinyi.

Mariam Mchonda ambae ni Hakimu Mfawidhi mkazi wa mahakama ya wilaya ya Ruangwa, amesema kutokana na kuwapo kwa changamoto hizo ndio maana katika wiki ya sheria wanapita katika kila tarafa kwa lengo la kuisaidia jamii kujua sheria mbali mbali ili iwe rahisi kufuatilia haki zao za kisheria pale wanapohisi hazijawafikia. Wiki ya sheria ilianza januari 22 mwaka huu ambapo inategemewa kuhitimishwa mwanzoni mwa mwezi Februari katika mahakama ya wilaya Ruangwa.