Ruangwa yapokea kilogramu 1500 ya mbegu za Alizeti
30 January 2023, 3:50 pm
Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi imepokea mbegu za Alizeti aina ya Record nbegu chotara (certified seeds) kilogram 1,500 kutoka Tasisi ya Agricultural Seed Agency (ASA) ya mkoani Morogoro.
Akizungumza baada ya kupokea mbegu hizo Afisa kilimo, Mifugo na Uvuvi Wilaya ya Ruangwa Norasco Kilumile, amesema kwa mujibu wa maelekezo ya Serikali mbegu hizo imeagizwa kuuzwa si zaidi ya Shilingi Elfu tano (5,000/=) kwa kilo moja na kuwaomba wananchi wote wenye uhitaji kujitokeza kujipatia mbegu hizo katika ofisi za Kilimo wilaya ya Ruangwa.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Ruangwa Ndg. Frank Chonya, amepongeza na kushukuru kwa upatikanaji wa mbegu hizo na kumuagiza Afisa kilimo kuhakikisha anaweka mfumo bora katika kuzigawa mbegu hizo kwa wakulima watakaojitokeza.