Tumieni mbolea muongeze tija katika kilimo
24 January 2023, 8:41 am
Wakulima wametakiwa kutumia mbolea ya ruzuku ya serikali ambayo huuzwa kwa thamani ya mfuko shilingi elfu Sabini (70,000/=) ili kuongeza tija ya uzalishaji katika sekta ya kilimo huku ikielezwa kuwa kilimo cha mazoea kinatajwa kuwadidimiza wakulima kupata mavuno haba.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Ruangwa Mh.Hassan Ngoma, 23Januari 2023 katiaka Ziara yake ya kata Kwa kata alipotembelea mashamba ya wakulima kata ya mandawa na chibula Wilayani Ruangwa mkoani lindi,ambapo amesema wananchi wanashindwa kuona tija ya kilimo na kujikuta wanalima bila mafanikio kwasababu hawatumii mbolea ya kupandia na kukuzia Kwa kuamini uwepo ya rutuba ya ardhi wanayotumia mara Kwa mara.
Baadhi ya wakulima waliotembelewa mashambani akiwemo Hamisi Chonjela na Hawa Japeleka wenye mchanganyiko wa mazao ya mahindi,mbaazi na mpunga wamedai gharama bado ni kubwa pia wameomba wataalamu wawape elimu ya kutosha ili kupata tija ya kilimo.