Ruangwa FM

Wazazi wapewa siku 4 Kuepeleka Watoto Shule

23 January 2023, 8:44 am

Mkuu wa wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi ametoa siku 4 Kwa wazazi na walezi kata ya mandawa na chibula kupeleka watoto ambao hawajaenda shule la sivyo karandinga kuwapitia.

Ngoma amezungumza hayo katika Ziara yake kata Kwa kata baada ya kupita na kukagua miradi ya shule na maendeleo ya uandikishwaji wa wanafunzi pamoja na kuzungumza na wananchi.

Hata hivyo DC Ngoma Amesema jumla ya wazazi 14 mpaka hivi sasa kata ya mandawa wapo lock up kwa makosa ya kutowajibika juu ya watoro wao ikiwamo kuwapeleka shule kwa wakati na kwamba ameeleza kuwa ni zoezi endelevu.

“kufikia ijumaa hujampeleka mtoto shule na wale wazazi watoto wao waliowaozesha umri mdogo,mimba za utotoni kufika ijumaa lock up utake usitake watoto ni wa serikali” alisema mkuu wa wiliya Hassan Ngoma.