Bilioni 32.1 zapitishwa Bajeti ya H/W Ruangwa Mwaka wa fedha 2023/24
21 January 2023, 9:47 am
Baraza la madiwani Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi, limepitisha Bajeti ya kiasi cha shilingi Bilioni thelathini na mbili milioni mia moja na saba laki saba na themanini na tatu elfu (32,107,783,000/=) kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024.
kwa mujibu wa taarifa ya kaimu Afisa Mipango Patson Masamalo aliemwakilisha mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, alipokuwa akiwasilisha bajeti hiyo amesema, fedha hizo zinakwenda kutumika katika maeneo mbali mbali ikiwamo, Mishahara ya watumishi,Matumizi mengineyo pamoja na Miradi ya maendeleo.
Wakichangia hoja baadhi ya madiwani na wajumbe waliohudhuria baraza hilo, katibu wa mbunge wa Jiimbo la Ruangwa, Kasambe Hokororo ameshauri ili mapato ya ndani yaongezeke ni vema kuongezwa kwa magaeti ya ukusanyaji mapato katika mipaka ya halamshauri ya aruangwa na halmashauri jirani akitolea mfano uvushaji wa mapato yanayokosekana katika mipaka ya kijiji cha nambilanje na nanjilinji ambapo hakuna kizuizi cha kukusanyia mapato.
” Halmashauri inafanya kazi vizurilakini nashauri maeneo ya mipaka yaongezwe vizuizi vya kuusanyia mamapto ili bajeti iweze kukamilika katikaukusanyaji wa mapato ya ndani, maan mapato mengi yanakosekana kwakua hakuna wakuanyaji hata kule nambilanje kwenda nanjilinji hakuna kizuizi ya ukusanyaji mapato” alisema kasambe alipokua anachangia katika baraza hilo.
Aidha katika hatua hiyo madiwaiwani wakiwamo Shabani kambona, Mosa mtojela na Rashidi Lipei wakahimiza bajeti kutekelezwa kwa mujibu wa maagaizo ya serikali ikiwamo fedha zilizotengwa za vijiji kiasi cha shilingi laki mbili katika kila robo ya mwaka zifike vijijini ili zikafanye maendeleo ya vijiji kama ilivyoagizwa na serikali, huku mkuu wa wilaya Hassan Ngoma akisisitiza kuwa fedha hizo lazima zipelekwe kwakua ni agizo la serikali na kwamba katika baraza linalofuat lazima ielezwe imefikia hatua gani kama zimeshapelekwa ama laa.
“kwakua ni agizo la serikali maana yake fedha hizo ni lazima zipelekwe katika vijiji na sio swala la hiari hivyo naagiza baraza lijalo tuletewe taarifa ya utathmini ni vijiji vingapi vishapelekewa fedha zake na vingapi havijapelekewa hizo fedha na kwa nini?” alisema Ngoma ambae ni mkuu wa wilaya ya Ruangwa.