Watoto wafundishwe kilimo- Chikongwe
17 November 2022, 3:52 pm
Mwenyekiti wa halimashauri ya wilaya ya ruangwa Andrew Chikongwe amewashauri watendaji WA kata na vijiji pamoja na madiwani kuweka mipango ya wanafunzi kufundishwa kilimo ili kuwajengea watoto uwezo mzuri wa kujifunza Maisha ya kujitegemea wawapo mtaani.
“Watendaji nendeni mashuleni watoto wafundishwe kilimo tunataka tuone gunia 20 Kwa ekar wananchi waone tunatengeneza kizazi kibaya mtu anamaliza degree hajielewi anazunguka tu na makaratasi tunawaanda kana kwamba wanaenda kukutana na computer mtaani wanazitoa wap?”Chikongwe
Chikongwe ameishauri Hilo katika kikao cha Baraza la madiwani cha robo yakwanza ya mwaka 2022/2023 Leo tarehe17 kilichofanyika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa wilaya ya ruangwa.
Aidha mwenyekiti huyo amesema mafunzo hayo yatasaidia pia katika ulaji wa wanafunzi mashuleni na kuondoa adha ya Wazazi kulalamika kila siku michango mashuleni kwani mashamba ya shule yapo
Madiwani na watendaji wameridhia Jambo Hilo kuanza kushawishi Wazazi na waalimu kupitia waalimu wa Masomo ya kilimo mashuleni kuwajenga vijana.