Kahama FM

Viongozi CCM kahama watakiwa kusikiliza, kutatua kero za wananchi

March 11, 2025, 3:46 pm

Katika ni mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi mkoa wa Shinyanga John Siagi ambaye ni mgeni rasmi, upande wake wa kulia ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama Thomasi Muyonga na Kushoto ni katibu CCM wilaya hiyo Andrew Chitwanga. picha na Sebastiani Mnakaya

Viongozi wa CCM kata kuacha tabia ya kuwafukuza makatibu wa matawi na mabalozi na badala yake wawafukuze wanaovunja utaratibu wa Chama kwa kuanza kupita kwa wajumbe kwa ajili ya kuwachagua tunapoelekea uchaguzi mkuu

Na Sebastian Mnakaya

Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga wametakiwa kuzitatua na kusikiliza kero ndogo ndogo zinazowakabili wananchi katika maeneo yao na wasie chanjo cha migogoro mbalimbali.

Haya yamesemwa leo na mwenyekiti wa Jumuiya wa Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga  John Siagi ambaye amemwakilisha Katibu mkuu wa Jumuiya hiyo Ally Hapi katika tamasha la kumpongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani kwa utekelezaji wa ilani ya CCM 2020-2025.

Siagi amesema kuwa kuna badhi ya wanachama kuanza kupita katika kata na majimbo kuomba kura ikiwa bado uchagunzi haujaanza na kuwataka kuacha tabia hiyo ili waliopo madaraki wafanye kazi.

Sauti ya mwenyekiti wa Jumuiya wa Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga  John Siagi

Aidha Siagi amewataka viongozi waliohudhuria katika hafla hiyo waendelea kuwajibika kikamilifu katika majukumu yao ili wawe mfano wa kuigwa katika jamii kwa utekelezaji Ilani ya chama cha Mapinduzi katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Sauti ya mwenyekiti wa Jumuiya wa Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga  John Siagi

Nae, katibu wa CCM wilaya ya Kahama Andrew Chatwanga, amewataka viongozi wa kata kuacha tabia ya kuwafukuza makatibu wa matawi na mabalozi na badala yake wawafukuze wanaovunja utaratibu wa Chama kwa kuanza kupita kwa wajumbe kwa ajili ya kuwachagua tunapoelekea uchaguzi mkuu.

Sauti ya katibu wa CCM wilaya ya Kahama Andrew Chatwanga
Wanancha wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Kahama wakiendelea kufatilia mkutano jinsi unavyoendelea. Picha na Sebastian Mnakaya

Leo Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Maponduzi (CCM) wilaya ya Kahama imempongeza mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt Rais Samia Suluhu Hassani kwa kuleta fedha nyingi katika mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendelea.