

March 6, 2025, 7:52 pm
Mbunge wa viti maalum kutokea mkoani Shinyanga Santiel Kiruma. picha Sebastian Mnakaya
Wanawake mkoani Shinyanga wahasa kujitokeza kwa wingi katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu ili kuongeza namba za wanawake kutoka asilimia 14% kwa sasa hadi kufikia asilimia 50%.
Na Sebastian Mnakaya
Wanawake wilayani Kahama wametakiwa kujitokeza kwa katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba mwaka huu kwa kugombea nafasi mbalimbili za uongozi.
Kauli hiyo imetolewa na Mbunge viti maalumu mkoa wa Shinyanga Santiel Kirumba wakati wa kongamano la wanawake lililofanyika katika kata ya Bugarama halmashauri ya Msalala.
Santile amesema wanawake wakipata nafasi katika uongozi wataweza kutatua kero za wananchi kwa sababu wanafahamu changamoto za jamii kwa kina
Aidha Santieli amewasisitiza wanawake kulipa umuhimu suala la tatizo la afya ya akili katika jamii ili kuondokana na athari mbalimbali zinazotokana na tatizo.
Wanawake mkoani Shinyanga wakiendelea kufatilia kwa umakini juu ya mafunzo ya afya ya akili
Naye, afisa maendeleo wa mkoa wa Shinyanga Rehema Edson, amesema takwimu za kimkoa mpaka sasa zinaonyesha wanaume katika nafasi za uongozi ni asilimia 86 huku wanawake wakiwa na asilimia 14% pekee.
Baadhi ya wanawake wakizungumza kwa nyakati tofauti katika kongamano hilo akiwemo Vumilia Migeka na Lucy Massawe wameeleza sababu zinazowafanya kutokugombea ikiwa ni pamoja rushwa ya ngono, elimu duni na mwanamke kudharauliwa katika jamii.
INSERT……..WANAWAKE KHM
March 8 kila mwaka dunia huadhimisha siku ya wanawake ambapo kwa mkoa wa Shinyanga maadhimisho hayo yameanza Machi 4 yakiwa na kauli mbiu “Wanawake na Wasichana 2025 tuimarishe usawa nauwezeshaji”