Kahama FM

Serikali mkoani Shinyanga yakemea biashara za magendo

March 1, 2025, 5:43 pm

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akiwa katika na viongozi mbalimbali wa mkoa huo

Serikali mkoani Shinyanga imewataka baadhi ya wafanyabia wanaojihusisha na biashara za magendo na kuzitaka mamlaka ya mapato Tanzania TRA pamoja na TAKUKURU kuchukua hatua za haraka ili kudhibiti vitendo hivyo.

Na Sebastian Mnakaya

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha ametoa onyo kwa baadhi ya wafanyabia wanaojihusisha na biashara ya magendo na kuzitaka mamlaka ya mapato Tanzania TRA pamoja na TAKUKURU kuchukua hatua za haraka ili kudhibiti vitendo hivyo.

Macha ametoa rai hiyo katika hafla ya kutoa shukrani kwa Walipa kodi bora kwa mwaka 2023/24 iliyoandaliwa na TRA mikoa ya Kikodi Kahama na Shinyanga iliyofanyika usiku wa Februari 28, 2025 Manispaa ya Kahama.

Macha amewataka baadhi ya walipa kodi wasiokuwa waaminifu katika kulipa kiwango sahihi na pasipo kudanganya ili kuendelea kuwa wazalendo kwa nchini yao, huku akiwataka kutokuwa na magendo kwa wafanyabiashara.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha

Aidha, Macha amewapongeza wafanyabiasha wa mkuo wa Shinyanga kuendela kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi pamoja na kwashukuru watumishi wa TRA kwa kuendelea kutoa huduma bora kwa kushirikiana na walipa kodi.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha

Awali akisoma risala kwa niaba ya Kamishna wa TRA, Emmanuel Nnko amesema mamlaka hiyo inaendelea na jitihada za kujijengea uwezo wa kupambana na baiashara ya magendo kwa kuboresha mafunzo kwa watumishi wake, kuongeza vitendea kazi vya kisasa ikiwemo vyombo vya usafiri majini na nchi kavu na kuendela kufanya msako maeneo husika.

Sauti ya kaimu kamishna wa TRA Emmanuel Nnkon

Mbali na hayo hafla hiyo pia imeambatana na utoaji wa tuzo kwa wapakodi bora wadogo, wa kati na wakubwa.