

February 28, 2025, 11:41 am
Naibu waziri mkuu na waziri wa Nishati Doto Biteki akiwa na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi CCM katika mkutano maalum Msalala( picha na Sebastian Mnakaya)
Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kushikamana na kushirikiana ili kuondokana na migogoro isiyokuwa ya lazima na badala yake waendelee kuwaletea wananchi maendeleo katika jimbo hilo
Na Sebastian Mnakaya
Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kushikamana na kushirikiana ili kuondokana na migogoro isiyokuwa ya lazima na badala yake waendelee kuwaletea wananchi maendeleo katika jimbo hilo.
Wito huo umetolewa na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko Dkt. Biteko katika Mkutano mkuu maalum wa Jimbo la Msalala uliolenga kupokea utekelezaji wa Ilani ya chama hicho katika kipindi cha mwaka 2020/25.
Dkt Biteko amewasihi Viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kahama kuacha tabia ya kuwa na makando kando na badala yake wakijenge chama hicho kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali ili kuendelea kutekeleza ilani ya cha cha Mapinduzi (CCM).
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo Mboni Mhita amesema kuwa miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa katika Halmashauri hiyo ikiwemo afya, elimu pamojana kuimarika kwa sekta ya madini.
Nae, mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kahama Thomas Muyonga, amesema kila mbunge katika jimbo lake ahakikishe amefanya maendeleo katika sekta mbalimbali kwa kutekeleza ilani ya CCM kwa jinsi inavyotakiwa.
Katika wilaya ya Kahama yenye majimbo matatu ya Uchaguzi ikiwemo Msalala, Ushetu na Kahama Mjini wamendelea kuwa na mikutano mikuu ya jimbo ili kila mbunge kuelezea namna alivyotekeleza ilani ya CCM kwa kipindi cha mwaka 2020/2025.