

February 22, 2025, 8:01 am
Dalili za ugonjwa wa Marbug huanza kuonekana kati ya siku mbili hadi ishirini na moja (21) baada ya kupatikana kwa maambukizi. Kwa mkoa wa Shinyanga hadi sasa hakuna mgonjwa Mwenye virusi vya Marburg.
Na Sebastian Mnakaya
Wananchi wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa marburg kwa kuzingatia hatua za kujikinga na kuwakinga wengine kwa kufuata taratibu na kanuni za afya ili kuondokana na maambuzi ya virusi vya ugonjwa huo.
Hayo yamesemwa leo na Mtaalam wa Magonjwa ya Mlipuko kutoka Hospitali ya Manispaa ya Kahama Dkt. Raphael Kibata, wakati akizungumza na Kahama FM, ambapo amesema ugonjwa huo ni hatari na wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari kwa kunawa mikono na maji yanayotiririka na kuachana kugusana na mtu mwenye dalili za ugonjwa huo.
Aidha, Dkt Kibata amesema kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama imeweka eneo la karantini kwa ajili ya mtu ambaye tayari amegundulika kuwa na ugonjwa huo, huku akiwataka wananchi kuchukua tahadhari wanapomuona mtu mwenye dalili ya ugonjwa wa marburg.
Nao, baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Kahama wakizungumza kwa nyakati tofauti, akiwemo Vicent Evalist na Samweli Binda wamesema wananchi wanauelewa mdogo juu ya ugonjwa huo na kuomba serikali kupitia wizara ya afya kuendelea kutoa elimu juu ya ugonjwa huo ili jamii iweze kufahamu