Kahama FM

Wauguzi na wakunga watakiwa kufuata taratibu na kanuni za Taaluma yao

February 18, 2025, 6:17 pm

Kaimu mganga mkuu wa serikali Dkt Saitole Laizer akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya kukabiliana na dharura za afya ya uzazi na watoto wachanga

Serikali itaendelea kutoa kushirikiano na wadau mbalimbali wa maendelea katika sekta ya afya ili kuboresha huduma za afya, huku akiwataka wataalumu wa afya kuzingatia maadili ya kazi.  

Na Sebastian Mnakaya

Wauguzi na wakunga pamoja na wataalamu wa afya nchini wametakiwa kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kuzingatia taratibu, maadili na viapo vya taaluma zao.

Wito huo umetolewa leo na Kaimu mganga mkuu wa serikali Dkt Saitole Laizer, akimwakilisha waziri wa afya Jenista Mhagama katika ufunguzi wa mafunzo ya kukabiliana na dharura za afya ya uzazi na watoto wachanga yaliofanyika katika manispaa ya Kahama, mkoani Shinyanga.

sauti ya Kaimu mganga mkuu wa serikali Dkt Saitole Laizer,

Naye, mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita, amewataka wauguzi na wakunga baada ya kupata mafunzo hayo waendee kuyafanyia kazi ili kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga, huku mwakilishi wa shirika la UNFPA Dkt Sundy Bukambila amesema mradi huo umelenga kuongeza na kupata wakunga wenye taaluma na wenye ujuzi

sauti ya mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita

Awali, akisoma risala Rais wa Chama Cha Wakunga Tanzania (TAMA) Beatrice Mwilike, ameiomba serikali kufanya mabadiliko katika muundo wa utumishi ili kumtambua mkunga katika ajira tofauti na ilivyo sasa.

sauti ya Rais wa Chama Cha Wakunga Tanzania (TAMA) Beatrice Mwilike,

Baadhi ya wahudumu wa afya ngazi ya jamii wilayani Kahama, akiwemo Simon Mihayo na Yohana Thomas wameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kushirikiana na wadau ya maendeleo kwa kupatiwa mafunzo ambayo yamewasaidia kushirikiana na wenza wao katika kipindi cha ujauzito mpaka kujifungua.

Sauti ya wahudumu