Kahama FM

Wananchi watakiwa kuboresha makazi yao baada ya kuvuna mazao

February 8, 2025, 3:29 pm

Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Ushetu

Baadhi ya wakulima katika halmashauri ya Ushetu ni duni hivyo katika kipindi cha masika nyumba hizo hudondoka kutokana na kuwa na kiwango cha chini cha ujenzi wake

Wananchi katika Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuboresha nyumba zao pindi wanapouza mazao baada ya msimu wa kilimo kumalizika ili kuepukana na majanga ya nyumba zao kubomoka kutokana na mvua.

Wito huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo, ambapo amebainisha kuwa bado baadhi ya wananchi wanaishi katika makazi duni hali ambayo inahatarisha maisha yao

mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita

Akizungumzia tukio la mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari chona kufariki dunia kwa kuangukiwa na ukuta wa nyumba aliyokuwa amepanga mkuu wa wilaya MBONI MHITA amemwaagiza wakuu wa idara kufanya ufuatiliaji wa wanafunzi ambao wanaishi katika nyumba za kupanga kujiridhisha iwapo ni salama

mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita