Kahama FM

Kahama wapiga marufuku viongozi wa mitaa kujihusisha na uuzaji wa viwanja

March 19, 2026, 4:48 pm

kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama Steven Magala akizungumza na wenyeviti wa mitaa ya Manispaa ya Kahama

Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga imepiga marufuku wenyeviti wa serikali za mitaa na vijiji kujihusisha na mikataba ya mauziano ya viwanja na maeneo kwakuwa ni kinyume na utaratibu wa sheria za manispaa.

Sebastian Mnakaya

Agizo hilo limetolewa na kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama Steven Magala wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kikao cha ndani cha wenyeviti hao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa manispaa hiyo.

Magala amewataka wananchi wanaohitaji kununua kiwanja wafike katika ofisi za ardhi manispaa ya Kahama ili kufuatilia kama eneo lipo halali a halina pingamizi lolote mahakamani au mgogoro wa mume na Mke.

Sauti ya kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama Steven Magala

Aidha, Magala amesema kuwa Manispaa ya Kahama imekuwa na migogoro mingi ya ardhi ambayo mingi ya migogoro hiyo inasababishwa na wenyeviti wa mitaa kushuhudia uuzaji wa viwanja mara mbili kwa watu wawili tofauti na wengine kushirikiana na wanunuzi wasio waamiifu.

Sauti ya kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama Steven Magala

Nao baadhi ya wananchi wa Manispaa ya Kahama wameipongeza manispaa ya Kahama kwa uamuzi huo na kwamba hali hiyo itasaidia kupunguza migogoro ya ardhi kwa wananchi hususan wanawake wajane ambao wanatapeliwa vwanja na nyumba zao mara kwa mara.