Kahama FM

Wanaume Kahama washauriwa kuwapeleka wenza wao kliniki

March 2, 2026, 12:43 pm

Jengo la wagonjwa wa nje Hosptali ya Manispaa ya Kahama. Picha na Tanzania yetu blog

Wanaume kuwapeleka wenza wao kliniki si jambo ambalo limezoeleka katika jamii, lakini ni muhimu kwa baba na mama kwenda cliniki pamoja kujua afya zao na kupata elimu kwa pamoja.

Na Faustine Mathias

Baadhi ya wananchi  wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameelezea umuhimu wa wanaume kuwapeleka wake zao wajawazito kliniki na kushiriki kikamilifu katika huduma za afya ya uzazi.

Wakizungumza  wananchi hao wamesema ushiriki wa mwanaume humtia moyo mama mjamzito na kumfanya ajisikie kuthaminiwa na kuungwa mkono katika kipindi hicho muhimu. Wameongeza kuwa mwanaume anapohudhuria kliniki hupata elimu sahihi kuhusu lishe bora, dalili za hatari, na maandalizi ya kujifungua salama.

Aidha wamesema kuwa baadhia ya wanaume wameanza kubadili mtazamo na kutambua kuwa ujauzito si jukumu la mwanamke pekee, licha ya kuwa baadhi yao majukumu huwafanya wasihudhurie

Kahama fm imezungumza na mmoja wa wahudumu wa afya ambapoamewataka wanaume kujitokeza katika kliniki za wajawazito, huku akibaninisha kuwa hatua hiyo inasaidia kupunguza hatari kwa mama na mtoto, pamoja na kuimarisha mshikamano wa kifamilia.

Sauti ya mhudumu wa afya

Hata hivyo, mwanaume Kumpeleka mwenza wake kliniki ni jambo muhimu kwa sababu linachangia afya ya familia, kuimarisha uhusiano wa ndoa, na kuhakikisha ustawi wa kijamii na kiafya.