Kahama FM
Kahama FM
February 23, 2026, 12:29 am

Wafanyakazi wa kampuni ya Costig Holdings ltd iliyopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kujua wajibu wao wawapo kazini pamoja na kuzingatia walichofundishwa na wataalum mbalimbali ili kuongeza uzalishaji zaidi.
Katika mafunzo hayo wataalumu kutoka sekta mbalimabli wakiwemo maafisa kutoka NSSF, Jeshi la zimamoto na uokaji Kahama, maafisa masoko kutoka Vodacom pamoja na walimu kutoka chuo kikuu SAUT wametoa mafunzo mbalimbali kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Mkurugenzi wa kampuni ya Costig Holdings ltd Stewat Bakuju, wamesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo ili kuwa na ufanisi wa kazi na wenye tija ili kuongeza masoko na uzalishaji.
Aidha, Bakuju amesema uzalishaji ukiongezeka utaweza kusaidia wafanyakazi hao kuongezewa mashahara, huku akiwataka kuwajibika kikamilifu katika utendaji wa kazi pamoja na kujua wanapaswa kufanya nini kazini.
Kwa upande wao, baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo, akiwemo Agnes Simon, Boniphace Mass na Gift Peter wameshukuru kupatiwa mafunzo hayo kutoka kwa wataalum mbalimbali ambao itawasaidia katika utendaji wao wa kazi pamoja na kujikinga na majanga mbalimbali yatakayojitokeza.

Naye, mkuu wa kituo cha zimamoto na uokoaji wilaya ya Kahama Hafidhi Omary, ametoa mafunzo namna bora ya matumizi ya gesi majumbani na viwandani pamoja na namna ya kukabiliana na majango yanapotokea.
Kampuni ya Costing Holdings ltd ilianzishwa mwaka 2002, na mapaka sasa inafanyakazi katika mikoa ya Shinyanga, Tabora, Geita, Kagera, Kigoma na singida, huku kwa wilaya ya shinyanga ina wakazi zaidi ya 31.