Kahama FM
Kahama FM
February 22, 2026, 12:40 pm

”Mkutano huo utatoa nafasi kwa wadau wa soka kubadilishana mawazo, kujadili changamoto na kuweka mikakati mipya ya kuendeleza mchezo wa mpira wa miguu nchini, ikiwemo ujenzi wa uwanja wa kisasa ambao utaweza kupokea zaidi ya watu 7,000”
Shirikisho la soka Tanzania (TFF) linatarajia kufanya mkutano mkuu wiki ijayo, ferbuar 27 na 28, 2026 wilayani ya Kahama mkoani Shinyanga, ikiwa ni kwa mara ya kwanza shirikisho hilo kufanyika mkutano mkuu wilayani humo.
Akizungumza na waandishi wa habari, katika Manispaa ya Kahama mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF Azan Mufti amesema kuwa kufanyika kwa mkutano huo, ni heshima kubwa na wakazi wa kahama na kuwataka kuchangamkia fursa kwa uwepo wa ugeni huo.

Mufti amesema mkutano huo utatoa nafasi kwa wadau wa soka kubadilishana mawazo, kujadili changamoto na kuweka mikakati mipya ya kuendeleza mchezo wa mpira wa miguu nchini, ikiwemo ujenzi wa uwanja wa kisasa ambao utaweza kupokea zaidi ya watu 7,000.
Aidha, ameongeza kuwa Rais wa TFF Wallece Karia anatarajiwa kuwasili Kahama Febuary 25 kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kabla ya kufanyika rasmi kwa mkutano huo.