Kahama FM

Baraza la Madiwani Manispaa ya Kahama lapitisha bajeti ya bil. 70

February 14, 2026, 10:57 am

Meya wa Manispaa ya Kahama Mataluma Kaniki akizungumza katika baraza la madiwani

Baraza la madiwa la Halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga limepitisha rasimu ya makisio ya bajeti shililingi bilioni 70 kwa mwaka wa fedha 2026/2027, fedha zitakazotumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya Manispaa hiyo.

Bajeti hiyo inatarajiwa kukusanywa kutoka katika vyanzo mbalimbali, ikiwemo mapato ya ndani, ruzuku kutoka serikali kuu pamoja na michango ya wananchi.

Mkuu wa idara ya Mipanga wa Manispaa ya Kahama Flora Sangiwa

Akiwasilisha rasimu ya bajeti, mkuu wa idara ya Mipango wa Manispaa ya Kahama Flora Sangiwa, amesema kuwa rasimu ya bajeti hiyo imepitia hatua zote za kisheria na kujadiliwa na kamati mbalimbali za halmashauri, huku ikijikita katika vipaumbe vya elimu, afya na miundombinu ya barabara.

Sauti ya mkuu wa idara ya Mipanga wa Manispaa ya Kahama Flora Sangiwa

Wakichangia bajeti hiyo, baadhi ya madiwani Manispaa ya hiyo, akiwemo diwani wa kata ya Iyenze Lucas Makulumo na diwani wa kata ya Mhungula Elisha William wamesema kuwa kuna maeneo ambayo ni muhimu, ikiwemo ununuzi wa mitambo ya ujenzi wa barabara yapatiwe kipaumbele katika bajeti hiyo pamoja na kwenye sekta ya afya.

Sauti za diwani wa kata ya Iyenze Lucas Makulumo na diwani wa kata ya Mhungula Elisha William