Kahama FM
Kahama FM
February 9, 2026, 12:44 am

Zaidi ya wananchi 63, 541 katika mkoa wa shinyanga kwa awamu ya kwanza watapatiwa huduma ya bima ya afya kwa wote bure kwa kaya zisizo na uwezo wa fedha, ikiwa gharama hizo zitalipwa na serikali.
Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita, katika kikao kilichowakutanisha wakurugenzi wa halmashauri, watendaji wa kata, madiwani na viongozi wa dini, ambapo amesema kuwa gharama za ukataji wa bima hizo utalipwa na serikali kwa kaya masikini.
Aidha, Mhita amesema kuwa mfumo mpya wa bima wa afya kwa wote utaweza kuwasaida wananchi walio na kipato cha chini, pamoja na kurahisisha upatikanaji wa huduma na kuongeza uwazi katika utoaji wa huduma za afya.

Nae, maganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Yuda Ndungile, amesema kuwa lengo la kuwa na Bima afya kwa wote ni wananchi kupata huduma hiyo pasipokuwa na kikwazo chochote wakati wa kupata huduma ya afya.
Kwa upande wao, baadhi ya waratibu wa TASAF wilaya ya kahama, akiwemo Witness Mlay wa Mansipaa ya Kahama na Richard Mwondya wa Halmashauri ya Msalala, wamesema zoezi la uwandikishaji kwa ajili ya Bima ya afya kwa wote linaendelea kwa wanufaika ambao ni kaya masikini kwa awamu ya kwanza.
Katika kuimarisha utekelezaji wa mpango wa Bima ya Afya kwa wote, serikali ya mkoa wa Shinyanga imejipanga kukagharima bima ya afya kwa kaya masikini 63,541 ambapo wilaya ya Kahama pekee inatarajiwa kunufaika kwa kaya 35,037.
