Kahama FM
Kahama FM
February 8, 2026, 5:23 pm

Mkuu wa wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Frank Nkinda amewaasa wanufaika wa mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri kuitumia vizuri kwa kuinua uchumi wao na zisiwe chanzo cha malumbano na ugomvi baina yao.
Nkinda ameyasema hayo wakati akikabidhi hundi ya Shilingi Bilioni moja na milioni kumi na mbili laki mbili na sabini na tatu elfu pamoja na baadhi ya vitendea kazi kwa vikundi vya vijana wanawake na wenye ulemavu katika Halmashauri ya Msalala.

Afisa Maendeleo ya Jamii Msalala Judica Sumari amesema lengo la mikopo na vifaa hivyo ni kuwezesha makundi hayo kujipatia kipato na kujiendeleza kiuchumi, Huku Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala Six Ibrahim amewataka wanufaika wa mikopo hiyo kurejesha kwa wakati ili kutoa fursa kwa wengine kukopa.
Kwa upande wa wanufaika wa mikopo hiyo Masanyiwa Kazinza pamoja na Lucia Saguda wameishukuru Serikali kwa kuwapatia Mikopo hiyo ambayo inaenda kuinua hali yao ya Uchumi.