Kahama FM

TARURA Kahama yatenga shilingi milioni 71.5 kwa ajili ya kukarabati wa barabara ya Mtakuja, Nyahanga

February 8, 2026, 4:28 pm

Diwani wa kata ya Nyahanga Josephina Kilimba akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani(Picha na Sebastian Mnakaya)

Wakala wa barabara wa mjini na vijijini (TARURA) wilayani Kahama mkoani Shinyanga, imetenga kiasi cha shilingi milioni 71.1 kwa ajili kufanya matengenezo barabara inayounganisha kata ya Nyahanga na Busonga.

Akizungumza katika baraza la mdiwani la Manispaa ya Kahama Kaimu meneja wa TARURA Kahama, Mhandisi Juma Masolwa, wakati akijibu swali la diwani wa kata ya Nyahanga aliyetaka kujua ni lini barabara hiyo itatengenezwa ili wanafunzi wasipate adha wakati wa kwenda shuleni.

Aidha, Mhandisi Msolwa amesema kuwa TARURA imetenga fedha kupitia tozo ya mafuta utakao karabati barabaro hiyo iliyokatika ili kuondokana na adha kwa wananchi na wanafunzi wanaoitumia barabara hiyo.

Sauti ya Kaimu meneja wa TARURA wilaya ya Kahama, Mhandisi Juma Masolwa
Kikako cha baraza la madiwani kikiendelea

Awali, diwani wa kata ya Nyahanga Josephina Kilimba akiuliza swali ndogo la nyongeza katika kikao cha baraza la mdiwani, ameiomba serikali kutengeneza barabara inayotekea Vatkani kuelekea shule ya msingi mtakuja mpaka manzese ili wanafunzi wasitembee umbali mrefu kuelekea shuleni.

Sauti ya diwani wa kata ya Nyahanga Josephina Kilimba

Hata hivyo, katika kipindi hiki cha mvua nyingi zinazoendelea kunyesha zimeleta athari kwa baadhi ya maeneo ya wilaya ya Kahama, barabara nyingi kuharibia na ngingine kukatika.