Kahama FM
Kahama FM
February 7, 2026, 1:32 pm

Mafunzo akiendelea kwa wafanyabiashara wa Kahama
”Mfumo wa IDRAS itawasaida wafanyabiasha kuondokana na gharama za kununu mashine za EFD kutokana na mfumo kutoa risiti”
Mfumo jumuishi wa usimamizi wa kodi za ndani(IDRAS) umelenga kuwasaidia wafanyabaisha kupata huduma ya risiti za EFD, kupita mfumo huo na kuondokana na kununua mashine za risiti.
Hayo yamesemwa na Afisa Msimamzi wa kodi, kitengo cha mawasiliano TRA Kahama Hamisi Sanze, wakati akizungumza na waandishi wa habara baadaya ya mafunzo kwa wafanyabiashara juu ya kuufahamu mfumo wa IDRAS aliyofanyika wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Aidha, Sanze amesema kuwa mfumo huo utawasaidia wafanyabiasha wengi katika masuala mbalimbali ikiwemo kuangalia madeni, pamoja na kujua namna ya ulipati wa kodi kwa wakati.

Kwa upande wao, baadhi wa fanyabiashara ya wilaya ya Kahama baada ya kupata mafunzo hayo, akiwemo Joyce Luleka na Idd Mwabululi wameeleza kuwa kupitia mfumo utawasaidia katika shughulizao za kila siku katika kuwahudumia wateja.
Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Kahama imekuwa na mwendelezo wa mafunzo kwa wafanyabiashara wa wilaya humo, katika kuufahamu mfumo w a IDRAS unaotarajiwa kuanza kutumika ferbuar 9, mwaka huu.