Kahama FM
Kahama FM
January 22, 2026, 2:00 pm

‘‘TARURA Kahama tunaomba mtenge bajeti kwa ajili ya kujenga mitalo ili kuondokana na changamoto ya kuharibika kwa barabara’’
Na Sebastian Mnakaya
Wakala wa Barabara Vijijini na Mjini(TARURA) wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kujenga mitalo pembezoni mwa barabara ili kuondokana athari za uharibu wa barabara katika kipindi hiki cha mvua.
Wito huo umetolewa na diwani wa kata ya Malunga Ahamed Haruni, wakati wa ziara ya mbunge wa jimbo la Kahama mjini Benjamin Ngayiwa katika kata hiyo, ambapo amesema barabara hizo ili ziweze kuwa nzuri na imara zinapaswa kujengewa mitalo.

Naye, Afisa tarafa wa Kahama Mjini Tumshukuru Mdui akimwakilisha mkuu wilaya ya Kahama, amesema kumekuwa na changamoto za ubovu wa barabara katika maeneo mengi ya Kahama, huku Halmashauri ya Manispaa ya Kahama ikitenga shilingi milioni 300 kwa ajili ukarabiti wa barabara hizo.
Kwa upande wake, kaimu meneja wa TARURA wilaya ya Kahama Juma Masolwa, amesema kuwa mpaka sasa wametenga bajeti kwa ajili ya maeneo ambayo barabara zinakatika kujenga mitalo ili kukabiliana na changamoto hiyo ya kuharibika kwa barabara.
Mbunge wa jimbo la Kahama na viongozi mbalimbali walitembelea katika kata ya Malunga Manispaa ya Kahama kwa ajili ya ukaguzi wa barabara baada ya mvua kunyesha.
